Saturday, December 30, 2017

Unaposikia Uwekezaji Katika Hisa Unapata Picha Gani?



“Mtu anayeuza hisa ni sawa na mtu anayeuza kuku wakati anapenda mayai” ~ Cypridion Mushongi
Neno "hisa" limekuwa maarufu sana miongoni mwa watanzania. Umaarufu wa neno hili umekua kutokana na kuenea kwa taasisi za VICOBA na SACCOS maeneo yote nchini yaani mijini na vijijini. Pamoja na watu wengi kuanza kushiriki zoezi la kununua na kumiliki hisa katika hatua mbalimbali, bado wengi wanakiri kuwa uelewa wao juu ya..

Monday, November 20, 2017

Unafahamu Makosa ni Mfuko Ulioficha Vitu Vizuri?




Kwenye mchakato wa biashara, ujasiriamali na maisha kwa ujumla, kuna makosa mengi yanayoendelea kufanyika. Wakati mwingine utulazimu kulipa gharama kubwa, ili kurekebisha makosa yaliyofanyika. Kwahiyo, tuseme kwamba makosa ni gharama, ndiyo maana wengi ujitahidi sana kukwepa kufanya makosa—Japo bado wanafanya makosa!! Lakini,

Monday, November 6, 2017

Kwanini Tunahitaji Umakini Kwenye Biashara?



 
Biashara au uwekezaji wowote unahitaji msingi imara, ili kuweza kukua na kuleta faida kwa mmiliki. Ukiwa na msingi imara kiwango cha hatari ya kushindwa kinapungua kwa kiasi kikubwa.

Chukulia mfano wa ujenzi wa nyumba; ukiwa unajenga nyumba unahitaji msingi imara, ili kuepuka nyumba yako kuanguka baadae. Ili kuufanya msingi wa nyumba yako kuwa imara, lazima unahitaji..

Monday, October 23, 2017

Athari za Kupenda Kuonekana Sahihi Mbele za Watu ni Hizi



 
Kuonekana umefanya makosa mbele za watu ni kitu kinachotishia utambulisho wa mtu, ndiyo maana watu wengi wanachukulia kufanya makosa kama jambo la kurudi nyuma. Mtazamo wa waliowengi ni kwamba kwenda mbele ni pale tu wenzako wanapokuona uko sahihi kwa mtazamo wao binafsi. Kutaka kuonekana sahihi mbele ya macho ya wenzako ndiyo usababisha

Monday, October 9, 2017

Monday, September 25, 2017

Kama Unaamini Pesa ni Sabuni ya Roho Soma Hapa


Ukweli ni kwamba watu wakipata pesa wanakuwa na furaha sana, kiasi kwamba ukikutana nao unaweza ukadhani ni watu wazuri sana, wanajali sana watu wengine, wana upendo kwa kila mtu. Kumbe yote mabaya yao mengi yanajificha ndani ya furaha itokanayo na kupata pesa. Kutokana na watu kuwa wachangamfu pindi wapatapo pesa, jamii yetu ya kitanzania ina msemo usemao..

Monday, September 18, 2017

Saturday, September 9, 2017

Umezaliwa Leo Kama Mimi Unafikiri Tutashinda Mchezo wa Maisha ya Pesa Lini?



Leo tarehe 9/9/2017 ni siku yangu ya kuzaliwa ambapo nimetimiza umri wa miaka 45 tangu nilipozaliwa. Baada ya siku ya leo, nitaanza safari yangu ya mwaka wa 46, nikiwa mwenye furaha hasa ninapoona kufikia hadi siku ya leo niko hai. Wakati huo huo, nazidi kuyalinganisha maisha yangu kama “mchezo wa mpira”. Maisha ni

Monday, September 4, 2017

Unajua ni Kwanini Tunalipa Pesa Kusoma kwa Lazima?


Katika kufikiria kwangu leo nimegundua kuwa kitu kinachoitwa chuo siyo majengo, viti, vitanda, godoro, walimu, nguo, chakula n.k. Vitu vyote vilivyotajwa vinapatikana majumbani mwetu. Lakini cha kushangaza bado tunakwenda chuoni, licha ya kwamba vitu vyote hivi bado vipo majumbani kwetu. Najiuliza ni kwanini tunaambiwa ni lazima

Monday, August 28, 2017

Fursa Nyingi Tuko Maskini Kwanini?


Mapema leo 28/08/2017, nilikuwa naangalia na kusikiliza video juu ya kongamano la wadau wa zao la mpunga, lililofanyika kuanzia tarehe 14-18 mwezi septemba 2015. Mkutano huo ulihusisha zaidi wanasayansi na wataalam wa kilimo cha mpunga. 

Katika mkutano huo, mmoja wa washiriki ambaye ni Profesa Nuhu Hatibu aliwasilisha mada yake iliyojulikana kama “Biashara ya kikanda kwa mazao ya chakula kama nyenzo ya kuufanya utafiti utumike katika kutengeneza utajiri” au kwa lugha ya Kingereza; “Regional Trade in Food Staples as an Instrument for Getting Research into use for Wealth Creation”. Katika video hiyo Profesa Nuhu Hatibu, alitoa nasaa za maana sana na akaeleza

Monday, August 14, 2017

Unajua Kwanini Kwanini Yako ni Muhimu?


"Kwanini yako" ndiye mlizi wako dhidi ya changamoto na wakatisha tamaa" ~ Cypridion Mushongi
Kwa mtazamo wa kimafanikio, kuweza kuuishi ukweli ni muhimu katika kufikia malengo yako hasa, uhuru wa kipatao/fedha. Jaribu kufikiria ulipokuwa bado mdogo, wakubwa zako walikuuliza unataka nini ukikua, pengine ulisema unataka kuwa mwanasayansi mashuhuri, mpishi, mwimbaji au daktari wa mifugo n.k. Na unaweza kukumbuka walionekanaje ulipowapa majibu hayo? Yawezekana walikukatisha tamaa kwamba haiwezekani au walikutia moyo kwa kukwambia kuwa unaweza ukawa mtu yeyote unayetaka kuwa, ilimradi

Monday, August 7, 2017

Sababu za Wateja Kuwa Zaidi ya Bosi ni Hizi Hapa


Katika maisha yetu ya kila siku, matendo yetu sikuzote yanadhihirisha na kuthibitisha kile tunachofikiri na kuwaza. Hii ndiyo kusema kwamba, kitu cha kwanza na muhimu kuwa na maisha bora yanayoambatana na uhuru wa kifedha ni jinsi tunavyofikiri na kutenda. Watu wengi wanafikiri mpaka watakapokuwa na mali nyingi ndipo watajiita au kujiona matajiri. Suala la kuwaza wengi wetu hatulipi kipaumbele, kiasi kwamba wengine wanadhani kukaa na kufikiri ni

Monday, July 31, 2017

Muuzaji na Mnunuzi Nani ni Mfanyabiashara?


Katika maisha yetu ya kila siku hapa duniani, kuna watu wanaofikiri na kuamini “sisi siyo wafanyabiashara wao ni wafanyabiashara”. Wengi wanaamini kuna kundi fulani la wafanyabiashara. Kutokana na mtazamo huu juu ya biashara, wengi wanajiaminisha kuwa wanaweza kuishi maisha mazuri bila kuwa wafanyabiashara. 

Watu wengi wanadahani mfanyabiashara ni

Monday, July 24, 2017

Hatari ya Kushindwa Kupanga ni Kama Hii



Nikiwa mmojawapo wa washiriki wa kikao cha kamati ya mradi wa kilimo siku ya tarehe 13/07/2017, mwenyekiti wa kamati alifungua kikao na kukumbusha wajumbe kuwa mojawapo ya majukumu ya kamati ni pamoja na kupanga namna bora ya uendeshaji wa shughuli za mradi. 

Katika kusisitiza hilo alisema “kushindwa kupanga ni kupanga kushindwa”. Maneno haya yalinigusa sana na yalinifanya kutafakari zaidi juu ya maana ya maneno haya katika maisha yetu ya kila siku.

Katika maisha kuna vitu ambavyo vipo na havitegemei uwepo wako. Vitu ambavyo havitegemei uwepo wako ni

Monday, July 10, 2017

Dawa ya Ujasiri wa Kukopa Pesa Benki Inapatikana Hapa



Kila ukigusia suala zima la watu kukopa pesa, wengi uonyesha wasiwasi wao mkubwa juu ya kitu mkopo. Kutokana na mtazamo uliopo juu ya mkopo, inaonekana kuwa mkopo ni kitu cha mwisho mtu kuweza kukifanya hasa hapa Tanzania. Ukweli ni kwamba jamii yetu imejaa woga juu ya mikopo hasa ile itolewayo na benki za biashara. Niseme kama wewe ni mjasiriamali wa kweli, uhitaji kuwa mwoga, bali

Monday, June 19, 2017

Tambua Viingiza-pesa Sahihi Kupata Uhuru wa Fedha





Habari njema ni kwamba kila mmoja wetu anayetafuta mafanikio ya kiuchumi amepewa uhuru na wigo mpana sana wa kuchagua njia na mbinu zitakazo mpeleka mpaka kufikia UHURU WA KIPATO (fedha). Unapoanza safari yako ya kutafuta “uhuru wa kipato” ni wazi kwamba ni muhimu sana kwako kuweza....

Monday, June 12, 2017

BAJETI ITAGUSA MAISHA YAKO UKIFANYA HAYA



Kila mwaka serikali inaposoma bajeti yake, watu wengi ujenga matarajio makubwa, ikiwa ni pamoja na wengi kutarajia kupata unafuu fulani katika maisha yao. Wengi uiangalia na kutathimini bajeti kwa mtazamo wa kupata mguso wa moja kwa moja kwenye maisha yao. 
Kikubwa kinachofuatiliwa kwenye kila bajeti, ni

Monday, June 5, 2017

Unaongeza Idadi ya Marafiki Wanyonyaji kwa Njia Hii



Katika Maisha ya binadamu ni kitu cha kawaida na muhimu kuwa na marafiki. Kwa karne nyingi, watu wametumia njia mbalimbali katika kuchagua marafiki wakuwanao karibu kila inapobidi. Katika kuchagua marafiki, wengi wetu tumekuwa tukitumia vigezo mbalimbali. Mfano ni

Monday, May 22, 2017

Tabia ya Pata Tumia Pesa Inakukwamisha Namna Hii


Kila tupatapo pesa, akiri yetu ututuma kutumia mara moja. Wengi wakishapata pesa, hapo hapo ujihisi kutokuwa na nguvu tena ya kuvumilia shida walizokuwanazo, kabla ya kupata pesa. Kuna wengine hata hawawezi kuvumilia walau masaa mawili bila kuwa wameanza kutumia pesa waliyopata. Kwa maneno mengine ni kwamba,

Monday, May 15, 2017

Jifunze Kwanini Tunasema Hakuna Makosa Duniani


Mojawapo ya vitu ambavyo vinachukiwa sana na binadamu ni kitu kinachoitwa “makosa”. Jambo hili la makosa linaogopwa sana kutokana na ukweli kwamba, wengi wetu tumekulia na kulelewa katika mfumo ambao ni watu wachache kwa nafasi zao wanaamua na kushawishi juu ya nini kifanywe na wengine ambao ni wengi.

Maana yake ni kwamba, watu wengi licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kuamua juu ya

Monday, May 8, 2017

Tunapanga Kuwa Masikini Namna Hii



Katika hali ya kawaida, kila binadamu anaishi kwa kupanga vitu vya kufanya. Katika zoezi zima la MPANGO, kuna makundi mawili ya watu. Kundi la kwanza ni watu waliopanga kutokuwa na mpango wowote wa maisha yao na kundi la pili ni

Monday, May 1, 2017

Leo ni Siku ya Wafanyakazi au Siku ya Wenyekazi Duniani


Kwa miaka mingi tumekuwa na utamaduni wa kupumzika na kusherekea eti! “sikukuu ya wafanyakazi” kila ifikapo tarehe moja mwezi Mei ya kila mwaka. Lengo au ajenda kuu ya siku hii ya leo, imekuwa ni kudai uboreshwaji wa maslahi ya watumishi (waajiriwa) kutoka kwa waajiri (wenyekazi).

Kusherekewa kwa siku hii ya “Mei Mosi” kunathibitisha mambo makuu mawili, ambayo ni

Monday, April 24, 2017

Kuchukia Makosa ni Kuchukia Masomo ni Kweli?



Siku zote watu wengi wanapojihisi kuwa wamefanya makosa, mara nyingi usikitika sana, ujawa na woga, wengine ukata tamaa ya kuendelea kufanya kile walichokuwa wakifanya. Lakini, ukweli ni kwamba

Monday, April 17, 2017

Monday, April 10, 2017

Habari Njema Kwa Wanaotafuta Ajira



Lengo lako la kutafuta ajira ni nini? Je? Ni kutafuta kulipwa mshahara? kutafuta mtaji? Au ni kwaajili ya kujifunza mambo fulani kama sehemu ya maandalizi ya kufanya kitu fulani hapo baadae? Kimsingi maswali juu ya malengo ya kutafuta ajira ni mengi sana.

Lakini ukichunguza kwa undani unagundua kuwa lengo kuu la watu wengi kutafuta ajira ni..

Monday, March 27, 2017

Pesa Inatakiwa Kuja Kwako Kwasababu Hii


Kila binadamu amezaliwa kama mchumi na anapaswa kuwa mchumiLakini, kwa wastani watu wengi siyo wachumi kwasababu hatujui thamani ya vitu ambavyo tayari tunavyo. Kuwa mchumi maana yake—siyo kuwa mbahili bali ni ile hali ya kuweza kupata matokeo makubwa kutokana na matumizi kidogo. Kazi ya kupata matokeo makubwa kutoka kwenye matumizi madogo si kitu cha hivi hivi bali ni..

Monday, March 20, 2017

Utajiri au Umaskini Utokana na Nini?



 


Kila mmoja ninaamini anao uwezo wa kuwa tajiri, isipokuwa binadamu huwa na fikra tofauti juu ya mambo yale yale. Kitu kilichoko akirini mwako ndicho kinacho leta tofauti ya hali ya Maisha unayoishi kwa sasa . Maana yake ni kwamba, jinsi ulivyo wewe ni zao la yale yote unayofikiri kila siku. Watu waliofanikiwa kuwa matajiri, wana mambo kama 5 ambayo wameyafanya kuwa kama kanuni zao za kudumu na kwakuwa ni kanuni, wao huzitekeleza na kuziishi kila siku. Kanuni zenyewe ni....

Monday, March 13, 2017

Ugonjwa wa Kuchoka Unatumaliza!


“Chanzo kikuu cha ugonjwa wa kuchoka ni watu wengi kufanya kazi ambazo hawazipendi” ~ by Cypridion Mushongi.
Ugonjwa ni hali ya kutojisikia vizuri, na wakati mwingine hali hii uambatana na maumivu makali sana. Katika ulimwengu wa afya, magonjwa yamegawanyika katika makundi makuu mawili. Kundi la kwanza ni magonjwa ya kuambukiza, mfano: kipindupindu, malaria, ukimwi n.k.

Kundi la pili ni

Monday, March 6, 2017

Ukibadili Unavyofikiri Hiki Kitatokea Maishani Mwako


"Hatuwezi kutatua matatizo kwa kutumia fikra zile zile zilizosababisha matatizo hayo kutokea" ~Albert Einstein


Ukweli ni kwamba, hatuhitaji pesa kubadili jinsi tunavyofikiri. Kwa maisha yetu yalivyo, sisi sote tuna uwezo wa kubadili jinsi tunavyofikiri bila kutumia gharama yoyote. Habari mbaya ni kwamba,...

Monday, February 20, 2017

Je ni Kweli Kila Tatizo Lililopo Duniani ni Biashara?



“Maskini anatumia muda wake mwingi kufanya kazi za watu wengine na akilipwa pesa anaitumia yote kununua suruhisho kutoka kwa watu wengine ili kutatua matatizo yake” ~ Cypridion Mushongi.
 
Kila wakati inapotajwa biashara, wengi wetu tunawahi kufikiri kuwa ni kununua vitu kwa bei ya chini na kuuza kwa bei ya juu. Hii siyo maana halisi ya neno “biashara”. Biashara ni..

Monday, February 13, 2017

Kiongozi Wako Mkuu ni Nani?


“Kama nina funguo za mlango wa asilimia 90 ya mafanikio yangu, sitajali sana endapo funguo za mlango wa asilimia 10 zitapotea” ~ Cypridion Mushongi.
 
Kuwepo kwa uongozi wa pamoja kumetupumbaza wengi kiasi kwamba watu wengi tumejenga tabia ya utegemezi wa fikra na mtazamo. Muda mwingi tumekuwa na matarjio makubwa kutoka kwenye uongozi wa pamoja. Lakini ikumbukwe kuwa uongozi wa pamoja au wa jumla unatokana na uongozi wa mtu mmoja mmoja. Bila kuimarika  kwa uongozi wa mtu mmoja mmoja, maisha..

Monday, February 6, 2017

Una Malalamiko Juu ya Biashara Yako?




"Tabia ya kulalamika inatokana na mfumo wa ajira ambao uwapa nafasi waajiriwa kupeleka malalamiko ngazi za juu endapo wanaona mambo hayaendi sawa---WAJASIRIAMALI TUSIWAIGE WAAJIRIWA"~ Cypridion Mushongi

Mbona unalalamika kila siku kwamba biashara yako ni ngumu? Kwani wewe ulianzisha biashara yako kwa lengo gani? Malalamiko kutoka kwa wajasiriamali imekuwa ni sehemu ya Maisha yao. Kila unapojaribu kuongea na wajasiriamali lazima usikie malalamiko mengi ikiwemo--

Sunday, January 29, 2017

Unajua Kwanini Kutaka tu Haitoshi?


"Ili kufanikiwa ni lazima hamu yako ya kubadirika iwe kubwa kuliko hamu ya kubaki ulivyo sasa" ~ Cypridion Mushongi

 
Neno “hamu” limekuwa likitumika visivyo. Mara nyingi, hamu imeelezwa kuwa ni “kile kitu tunachofikiria kupata” Hapana. Hamu ni...

Thursday, January 19, 2017

Unafahamu ni Kwanini Uko Hivi Ulivyo?


“Uwezo wako wa kutawala na kupambana na changamoto za dunia, una uhusiano wa moja kwa moja na jitihada unazoziweka katika kukamilisha kazi~ Cypridion Mushongi

 

Kila binadamu amepewa uwezo mkubwa kama zawadi kwaajili ya kukuwezesha kupata kitu chochote atakacho maishani. Lakini, ili zawadi yako ya uwezo ikunufaishe, unahitaji kufanyia kazi uwezo wako. Ukweli ni kwamba tumepewa uwezo kama zawadi na wakati huo huo kama amri kwasababu,

Thursday, January 12, 2017

Hii ni Njia Sahihi Kujipatia Uhuru wa Fedha




"Usikae kitandani mpaka pale utakapoweza kutengeneza pesa ukiwa kitandani" ~ George Burns
 
Mchakato ni mpangilio wa shughuli mbalimbali ambazo ufanyika hatua kwa hatua mpaka kufikia hatua ya kutoa matokeo yaliyolengwa. Kwa maneno mengine, kitu mchakato ni zaidi ya kukamilisha shughuli moja na hii ndiyo tofauti kubwa kati ya mchakato na shughuli.

Kwa mfano; ukiambiwa kuwa kutajirika ni mchakato, basi fahamu moja kwa moja kuwa utahitajika kufanya shughuli nyingi hatua kwa hatua kwa kipindi kisichopungua miaka

Sunday, January 8, 2017

Je? Wewe ni Mwekezaji au Mfanyabishara



"Soko la hisa ni kifaa cha kuhamisha pesa kutoka kwa watu wasiokuwa na subira kwenda kwa wenye subira” ~ Warren Buffet.

Kwa mwaka huu wa 2017, unahitaji mwanga ili pale palipokuwa hapaonekani paonekane na wewe ikuwie rahisi kupita kwa lengo la kwenda kwenye mafanikio hasa ya uhuru wa fedha (kipato). Ukweli ni kwamba huwezi kufikia maisha ya kiwango cha kupata uhuru wa fedha au kipato kama bado..