Saturday, December 31, 2016

Fungua Mwaka ya Uchumi ni Hii Hapa



 
Mahitaji ya binadamu ni mengi sana na hayana kikomo. Mahitaji haya yamegawanyika katika makundi makuu mawili yaani “Vitu/Bidhaa” na “Huduma”. Pamoja na mahitaji mengi ya binadamu, mtu mmoja mmoja hawezi kuzalisha na kujitoshereza kwa kila kitu. Ndiyo maana binadamu wengi uendesha maisha yao kwa

Sunday, November 13, 2016

Je? Unatafuta Utajiri Au Unaangaika Kuwa Maskini


“Mtu aliye na tabia ya kuangaika vile vile ana tabia ya kutaka kila kitu apate leo leo, mwisho wake anaambulia kupata vitu vidogo vidogo” ~ Cypridion Mushongi
 
Leo wakati natafakari juu ya utajiri, nimekumbuka sana mwanzoni mwa miaka ya 2000. Miaka hiyo nilikuwa na rafiki yangu ambaye alizoea kusema “Mwaga mtama kumkamata kuku kirahisi na usiangaike kumkimbiza kuku unaweza kuvunjika mguu kabla ujamkamata”. Ni kawaida kukuta watu wakikimbiza kuku pindi wanapohitaji kitoweo. Hali hii huwafanya wengine kuumia kwasababu ya kutumia nguvu nyingi kupita kiasi.

Tabia ya kumkimbiza kuku kila mara tunapohitaji kitoweo, inafanana sana na tabia tuliyonayo katika kutafuta utajiri. Ukifuatilia kwa undani utagudua kuwa michakato yetu ya kutafuta utajiri ni

Sunday, November 6, 2016

Tofauti ya Kuwa Tajiri na Kuonekana Tajiri Iko Hapa


“Dawa ya kutibu ugonjwa wa kujiona tajiri ni kuweka ndoto ya maisha mazuri unayoyataka kwa maandishi” ~ Cypridion Mushongi
Katika mchakato wa kutafuta utajiri kuna dhamira kuu mbili zinazotuchochea kufanya kila tunachokifanya, ili kutimiza ndoto ya kutajirika. Dhamira ya kwanza ni ile mtu anapolenga kuonekana tajiri machoni mwa watu wengine na dhamira ya pili ni

Saturday, October 22, 2016

Jinsi ya Kuwa Mkubwa Kuliko Matatizo

“Utasonga mbele tu pale utakapoacha kujibinafsisha matatizo yanayoendelea kutokea katika mchakato wa maisha yako” ~ Cypridion Mushongi


Njia mojawapo ambayo ni kisababishi kikubwa cha hisia hasi na hasira ni hali ya kupenda kujibinafsisha au kujimilikisha matatizo yanayoendelea kutokea. Tabia au hali hii ya kupenda kujibinafsisha ni...

Wednesday, October 12, 2016

Biashara Yako Inakutaka Ufanye Yafuatayo



 "Kila utakapoona biashara iliyofanikiwa ujue kuna mtu alifanya maamuzi ya kijasiri" ~ Peter F. Drucker

Watu wengi tunatamani sana kuwa matajiri, lakini wengi wanakata tamaa. Mojawapo ya njia muhafaka itakayotufikisha kwenye utajiri ni “biashara”. Biashara ni

Thursday, October 6, 2016

Utaweza Kuondoa Chuki na Hasira Ulizonazo Kwa Njia Hii


“Nimeamua kujikita kwenye UPENDO...Chuki ni mzigo mkubwa sana kuubeba” ~ Martin Luther King Jr.
Unapoona watu wanatembea, wanaongea na wanacheka, usidhani wengi wana furaha ya dhati. Ukweli ni kwamba watu wengi wana chuki, hasira, kinyogo na kero nyingi ndani yao. Kubwa zaidi ya yote ni kwamba..

Saturday, September 24, 2016

Mambo Manne ya Lazima Mjasiriamali Kuyajua


“Utajiri unapendelea wale walio na ujasiri!” ~ Cypridion Mushongi
Mjasiriamali wa kweli sharti ajiongoze mwenyewe katika kufanya maamuzi juu ya biashara yake au maisha yake kwa ujumla. Ili, mjasiriamali ajiongoze vyema, ni muhimu ajitahidi kujifunza masuala mbalimbali yanayogusa kile ambacho anakifanya au anatarajia kukifanya. Kwa kawaida, hatutegemei mjasiriamali wa kweli afanye kazi kwa...

Friday, September 16, 2016

Fahamu Kwanini Kesho si Rafiki wa Mafanikio Yako





Katika maisha yetu ya kila siku,  neno “kesho” linatumika sana kama njia pekee ya kuhairisha mambo mengi, ambayo kimsingi yalitakiwa yafanyike “leo”. Kesho ni miongoni mwa maneno yanayopendwa kutumiwa kama kinga ya kukataa kutimiza majukumu fulani ya leo. Badala ya mtu kusema “HAPANA” kitu hiki, anajibanza nyuma ya...

Friday, September 9, 2016

Miaka 45 ya Kuzaliwa Tumezeeka au Tumekua?




Mara nyingi watu wengi tunapozeeka udhania kwamba tumekua kumbe ndio kwanza tunazidi kuwa watoto wachanga. Mafanikio makubwa yanapatikana kwa urahisi kwa wale tu waliokua na si waliozeeka.  Ukikua ndipo unapata-

Friday, September 2, 2016

Mwajiriwa Jilipe Kwanza Mjasiriamali Ufanye Nini?


"Sisi kama wajasiriamali wa kweli lengo letu la kuanzisha biashara sio kwaajili ya kupata MSHAHARA bali ni kujenga VIINGIZA-PESA~ Cypridion Mushongi


Sifa kuu ya mwajiriwa huwa ni kulipwa “mshahara au ujira”. Maana yake ni kwamba yule aliyekuajiri anawajibika kukulipa muda wako ambao umeutumia kwenye biashara yako. Haijalishi mshahara wako ni mkubwa au mdogo kiasi gani bali mshahara wako ni..

Sunday, August 28, 2016

Mjasiriamali Tanzania ni Nani?



Neno mjasiriamali ni miongoni mwa maneno yanayotamkwa sana kila siku, hapa Tanzania. Kwa hali iliyopo hivi sasa, ni kana kwamba wajasiriamali ni wengi sana Tanzania. Sababu ya kudhani kwamba kuna wajasiriamali wengi ni..

Tuesday, August 23, 2016

Utajiri Wako Unachelewa Kwasababu Moja






Kwa jinsi binadamu tulivyo, tunaweza kuona vitu vyote ambavyo havionekani mbele ya macho yetu. Ukifuatilia kwa undani unagundua kuwa vitu ambavyo tunaambiwa na kuamini kuwa havionekani, kiuhalisia vitu vyote vyaweza kuonekana endapo ukiamua. Kwa mazoea, wengi tunafikiri kwamba kama kitu hakionekani mbele ya macho yetu ya kawaida, basi tunasema...

Sunday, June 26, 2016

Pesa Haihitaji Mtaji Kuipata ni Kweli?


Kila ninapojaribu kushirikisha rafiki zangu juu ya dhamira yangu ya kufanya mambo makubwa maishani kama vile kuwa kati ya mabilionea wakubwa 10 nchini Tanzania, huwa ninapata jibu la “huwezi”, kwamba hayo ninayotaka kuyafanya yanataka mtaji mkubwa sana. 

Hatahivyo, nimeapa kutokata tamaa, kwasababu wanasema “mtu akikwambia huwezi kufanya hili” maana yake...

Tuesday, June 21, 2016

Pesa Inaingia Mfukoni Ukijua Lugha Yake ni Ipi Hiyo?


“Watu wengi wanatumia pesa walizopata..kununua vitu wasivyovihitaji..kufurahisha watu wasiowapenda” ~ Will Rogers

Mojawapo ya nguzo muhimu katika kupata maisha mazuri ni pesa ya kutosha kumudu gharama za maisha ya kila siku. Zaidi ya hilo, ni kwamba mafanikio binafsi ya kifedha ni chachu ya mafanikio ya aina nyinginezo. Lakini...

Tuesday, May 31, 2016

Mbinu Hizi za Kupata Pesa Zinakufaa



 "Visingizio ndio misumari ya kujenga daraja la kushindwa" ~ Cypridion Mushongi

 

Kupata pesa kunahitaji vitu vingine zaidi ya pesa. Vitu vingine zaidi ya pesa ni pamoja na wewe kufahamu na kujifunza tabia na mbinu mbalimbali wanazotumia wale waliofanikiwa tayari. Kwakusoma makala hii tayari umekwisha anza safari yako ya kutengeneza pesa nyingi na hatimaye kuishi maisha ya ndoto yako.

Ni vizuri safari yako ikaanza kwa kufahamu kwanza mbinu hizi tisa ambazo ni muhimu ukazitumia katika harakati zako za kujenga utajiri kwa sasa na siku za usoni.
 Mbinu hizi ni

Wednesday, May 25, 2016

Hii Ndiyo Hasara ya Kulipa Kwanza Watu Wengine


“Unapopata pesa ukatenga akiba kwanza, tunasema umejilipa kwasababu pesa hiyo imebaki kwako na ndiyo mbegu ya kuzalisha pesa nyingi zaidi” ~ Cypridion Mushongi
 
Watu wengi tunajua kuwa ukishafanya kazi ya mwajiri kinachobakia ni kulipwa mshahara au ujira, nje ya hapo hatuna habari. Ukilipwa na mwingine unafurahi sana. Furaha unayoipata ukiwa umelipwa mshahara, pengine ndiyo inakusukuma kutumia mara moja kipato chako kila unapolipwa. Hali hii ya kufurahia kulipwa pesa na wengine ndiyo imezidi kutuweka utumwani maisha yetu yote.

Kila tunapolipwa pesa, kazi yetu ya kwanza huwa ni

Wednesday, May 18, 2016

Elimu ya Pesa Yaanza Kupatikana


"Mwanzo wa kutajirika ni pale utakapojua mwelekeo wa matumizi ya pesa yako, ama ni zaidi kwa viingiza pesa au ni zaidi kwa vitoa pesa!"  ~ Cypridion Mushongi

Watu wazima tuliowengi sasa hivi tunajua kusoma na kuandika. Tumepitia kwenye njia na hatua nyingi, ikiwa ni pamoja na kutumia gharama kubwa kwaajili ya kutafuta kuelimika na kufuta ujinga tuliokuwa nao. Tunamshukuru Mungu, hicho ni kitu kimoja ambacho shule zetu zinakifanya vizuri. Lakini,...

Wednesday, May 11, 2016

Ukweli Kuhusu Mwekezaji ni Huu


“Usitegemee kipato kutoka kwenye chanzo kimoja peke yake BALI wekeza ili kutengeneza chanzo cha pili” ~ Warren Buffet
 
Bilashaka wewe unayesoma makala hii, umesikia mara nyingi maneno kama “uwekezaji, mwekezaji n.k. Pengine niseme kuwa, kwa nchi kama Tanzania ambayo iliwahi kuongoza na kuendesha siasa zake pamoja na uchumi wake kwa kufuata falsafa na kanuni za mifumo ya ujamaa na hata ukomunisti, neno “uwekezaji na wawekezaji” ni vitu ambavyo ni vigeni na vinachukuliwa kuwa ni kazi ambazo ni maalum kwa wazungu!. Watanzania wengi bado hawaamini kama mtanzania tena ambaye ni

Saturday, April 30, 2016

Umuhimu wa Kutafuta Pesa Bila Sababu ni Huu


“Unashindwa kupata pesa nyingi kwasababu unatafuta pesa kulingana na shida unazotegemea kupata siku zijazo” ~ Cypridion Mushongi
Siku moja nilikuwa naongea na rafiki yangu ambaye aliwahi kuniuzia kiwanja siku za nyuma. Baada ya mwaka mmoja tangu rafiki huyo aniuzie kiwanja, tulikutana mjini Bukoba na hapa aliniuliza juu ya mpango wangu wa kukiendeleza kiwanja hicho. Jibu langu kwake lilikuwa...

Friday, April 22, 2016

Siri ya Watu Kupenda Mikate Imefichuka



“Kama pesa ni kazi iliyoisha, wewe pesa yako kazi yake imefanywa na nani?” ~ Cypridion Mushongi
Jumapili ya tarehe 17/04/2016…nilikuwa nyumbani nasikiliza mziki wa injiri, mara tu ukapigwa wimbo wa “Mikate” ambao umeimbwa na “AIC Chang’ombe Vijana Kwaya”. Katika wimbo huu waimbaji wanasikika wakiimba kuwa “Watu Wanapenda Mikate” . Wimbo huu umebeba ujumbe mzito na unaeleza.....

Tuesday, April 12, 2016

Pesa ni Matokeo Nifanye Nini?



Matokeo ni kitu kizuri kwani kinapendwa karibu na kila mtu. Matokeo ni kitu cha mwisho kutokea baada ya hatua mbalimbali na shughuli nyingi kufanyika. Kwa maana nyingine tunaweza kusema kuwa pesa ni hitimisho. Matokeo yana sifa moja nayo ni...

Tuesday, April 5, 2016

Wewe au Pesa Nani Kashuka Thamani?


“Bei ni kile unacholipa. Thamani ni kile unachopata” ~ Warren Buffet
Wimbo ulioenea kote nchini sasa hivi ni “kushuka thamani ya pesa au shilingi ya Tanzania”. Watu wengi tunashusha lawama kwa watu waliopewa madaraka hasa ya kuongoza taasisi za kifedha. 

Lakini nimetafakari sana jambo hili. Fikra na imani yangu vinanituma kuamini kuwa....

Tuesday, March 29, 2016

Unapata Faida Gani Kwenye Woga?



 "Kitu pekee tunachoweza kuogopa ni woga wenyewe" ~ Franklin D. Roosevelt



Jiulize leo: “Ni faida kiasi gani unaweza kutengeneza kutokana na woga?. Na hii ndiyo sababu ya kwanini nimelazimika kuangalia moja kwa moja kwenye macho ya “WOGA” bila woga.....

Neno woga...

Saturday, March 19, 2016

Elimu ya Ujasiriamali Haipo Chuoni Iko Wapi?

“Usione aibu kutokana na kushindwa, jifunze kutokana na kushindwa na uanze tena” ~ Richard Branson, mwanzilishi wa kampuni ya Virgin Group.

Mara nyingi shuleni tulifundishwa kutii sheria na taratibu kama siyo kanuni; kufanya vitu kwa kutumia vitabu na kama ukionekana ukikaa mbali na kundi, haraka haraka unasukumwa tena kwenye tanuru ambalo hasa ni......

Tuesday, March 15, 2016

Ukiendelea Kutafuta Muda Utazidi Kuhailisha Mengi ya Muhimu!


“Muda ni bure lakini huwezi kuuza kwa bei yoyote, huwezi kuumiliki lakini unaweza kuutumia, Huwezi kuutunza lakini unaweza kuupoteza, ukishakuwa umeupoteza huwezi kuupata tena” ~ Harvey Mackay
 
Watu wengi tuko busy sana katika kutafuta muda eti! Wa kufanya mambo makubwa maishani. Lakini imeonekana kuwa pamoja na kutafuta muda, bado haupatikani kirahisi, kwani malalamiko ya watu kuhusu kukosa muda wa kutenda kazi mbalimbali ni mengi.

Nadhani na wewe umesikia mara nyingi watu wakilalamika kuwa wanashindwa kufanikisha jambo fulani kwasababu ya uhaba wa muda. Malalamiko haya yanatokana na.....

Wednesday, March 2, 2016

Siri ya Faida Kuwa Bora Kuliko Mshahara Imefichuka


“Lengo la biashara yoyote ni kutoa suruhisho ya matatizo ya watu-kwa FAIDA” ~ Paul Marsden
Pesa ambayo huwa tunapata mara zote utoka kwenye mifumo mikuu miwili ambayo ni “mfumo wa mshahara” na “mfumo wa FAIDA”. Kati ya mifumo hiyo, mfumo wa mshahara ndio unaotegemewa na kuaminiwa na watu wengi. Lakini...

Friday, February 26, 2016

Fahamu Kwanini Tunasema Muda Siyo Tatizo!



“Kila mtu anatenga muda mwingi kufanya kazi anazotaka zifanyike na hatengi muda kabisa kufanya kazi ambazo hataki”.
Imekuwa ni kawaida watu wengi kulalamika kuhusu kutokupata muda wa kufanya shughuli fulani fulani. Nadhani ni mara nyingi umesikia kauli za kulalamikia ukosefu wa muda wa kufanya kazi fulani fulani. Malalamiko haya, yanatokana na.....

Tuesday, February 23, 2016

Unajua Kwanini Pesa ni Ngumu Kupatikana?



“Kutokuwa na pesa ni chanzo cha mabaya mengi” ~George Bernard Shaw.


Binadamu ili apate kufahamu kitu fulani lazima picha iliyoko kichwani ilingane na kufanana na kitu unachotafuta. Endapo picha zikipishana lazima itakuwa vigumu sana kupata hicho unachotafuta. Mara nyingi, tatizo hili la kupishana kwa picha linatokea zaidi kwa vitu vingi ambavyo siyo....

Friday, February 19, 2016

Unadhani Pesa Uliyonayo ni Kidogo au Nyingi?



 "Mungu hakupi pesa kidogo au nyingi, anakupa tu kile kiasi unachohitaji”.



Kwasasa wapo watu wengi wanaodhani kuwa wao wanazo pesa kidogo na wangependelea Mungu awaongezee. Pia kuna wale wachache ambao wanadhani wanazo pesa nyingi lakini.......

Tuesday, February 16, 2016

Hii Ndiyo Faida Upatayo Ukikubali Mtoto Awe Mwalimu Wako



“Watu waliofanikiwa sana katika maisha ni wale ambao upenda kuuliza maswali. Wanajifunza kila wakati. Wanakua kila wakati. Wanajisukuma mbele kila wakati.” – Robert Kiyosaki
 

Mwaka 2013 nilialikwa na kushiriki katika sherehe ya jubilee ya Baba Askofu Dk. Benson Bagonza wa KKKT Dayosisi ya Karagwe. Jubilee hiyo ilikuwa ni ya kutimiza miaka 50 ya kuzaliwa kwake, miaka 20 ya ndoa na miaka 10 ya uaskofu. Sherehe hiyo ilitanguliwa na ibada maalum ambayo iliongozwa na Baba Askofu mwenyewe.

Katika mahubili yake siku hiyo.....

Tuesday, February 9, 2016

Muda wa Ziada Utakukwamua Namna Hii


“Yale unayofanya wakati wa muda wako wa ziada ndiyo yanakuweka huru au utumwani” ~Jarod Kintz
 

Utafiti uliofanyika duniani umeonyesha kuwa wengi wa wajasiriamali waliofanikiwa, walianza biashara zao kwa kutumia muda wao wa ziada. Ni mara ngapi umesikia mtu akisema “ningependa kufanya biashara hii LAKINI tatizo sina muda?” Unapoona mtu akwambia sina muda maana yake ni....

Saturday, February 6, 2016

Njia Mpya ya Kununua Muda Wako Tena Imefahamika


“Falsafa ya matajiri na masikini ni hii hapa: Matajiri wanawekeza pesa yao na kutumia kiasi kinachobaki, Masikini wanatumia pesa yao na kuwekeza kiasi kinachobaki” ~ Robert Kiyosaki
 
Hali ya umaskini katika jamii yetu kwa kiasi kikubwa imesababishwa na watu wengi kuuza muda wao kwa watu wengine. Dunia ya leo bado inatawaliwa zaidi na kundi la watu ambao biashara yao ya kila siku ni kuuza muda kwa lengo la kujikimu kimaisha. Katika ulimwengu wa kutafuta riziki (kipato), tunapata kuona aina kuu tatu za kipato ambazo ni.....

Wednesday, February 3, 2016

Kuishi Maisha ya Chapati ni Hatari Tupu!



“Umaskini Unakuja Kwako Bila Gharama Yoyote LAKINI Unaondolewa kwa Gharama Kubwa Sana”


Chapati ni bidhaa ambayo ni chakula tunachokipenda sana na pia ni bidhaa inayokubalika na kuhitajika kwa kiasi kikubwa katika maeneo mengi ya hapa nchini Tanzania. Lakini......

Friday, January 29, 2016

Je ni Kweli Uzoefu Unaleta Woga?


“Kila kitu kipya ambacho unaweza kufikiri ni HALISI hata kama hakijawahi kuwepo” ~ Pablo Picasso ~

Uzoefu ni elimu au uelewa fulani ambao mtu anakuwanao kutokana na kufanya kazi mbalimbali lakini mara nyingi ni.....

Tuesday, January 26, 2016

Unataka Kutajirika Anza na Hili

“Uhuru wa kipato upo kwa wale tu waliotayari kujifunza na kufanya kazi” ~ Robert Kiyosaki
Watu wengi wanatafuta utajiri kwa hudi na uvumba, japo wengine wachache wanapata na waliowengi wanakosa na kukata tamaa. Jambo ambalo ni dhairi kabisa ni kwamba, watu wengi tunaanza safari ya kutafuta utajiri katika hatua au vituo tofauti tofauti. Kwahiyo, swali la kujiuliza ni je? Safari yetu ya kutafuta Utajiriinapaswa kuanzia...

Friday, January 22, 2016

Jitahidi Upate Kusoma Kitabu Hiki



“Mimi siyo zao la hali yangu ya maisha BALI ni zao la maamuzi nifanyayo kila siku”. ~ Stephen Covey ~

Ukibahatika kupata na kusoma kitabu cha “Are you fully charged?” Utajifunza mambo makubwa sana ambayo yatarahisisha kazi yako ya kusaka mafanikio makubwa.

Kutoka katika kitabu hiki na mimi nimejifunza mambo mengi sana LAKINI nimeona nikushirikishe mambo 5 kama sehemu ya mambo niliyojifunza kutoka katika kitabu hiki: Mambo 5 niliyojifunza mimi binafsi ni….

Tuesday, January 19, 2016

Hii Ndiyo Hatari ya Kukwepa Kukataliwa



“Nachukulia kukataliwa kama mtu anayejaribu kupigia tarumbeta kwenye masikio yangu ili kuniamsha niendelee na safari badala ya kurudi nyuma”
~ Sylvester Stallone ~

Katika ulimwengu wa nafsi kuna watu wa aina mbili. Kundi la kwanza ni wale watu wenye kumiliki nafsi zao, kundi hili tunaweza kuwaita “Wamiliki”; na kundi la pili ni................

Friday, January 15, 2016

Huu Ndio Muujiza wa Makosa



“Mtu yeyote ambaye hajawahi kufanya makosa, ni yule ambaye hajawahi kujaribu kitu chochote kipya” ~ Albert Einstein ~
 Mpendwa msomaji wa MAARIFA SHOP ni kwamba kuna kitu kama muujiza karibu kwenye kila kosa lifanyikalo katika maisha yetu ya kila siku. Na muujiza huu unaitwa....

Wednesday, January 13, 2016

Wakati Unatafuta Ajira Fahamu Jambo Hili…..


“Maandalizi mazuri ya kazi nzuri ya kesho ni kufanya kazi nzuri leo”
~ Elbert Hubbard

 
Kati ya changamoto kubwa tunayopitia kwenye dunia ya sasa ni kwamba kila mtu ana fikra na maoni yake. Na kutokana na hali hii, watu wengi wamekuwa wakichukua maoni wanayopewa na kufikiri ndio ukweli. Lakini...

Friday, January 8, 2016

Safari Mpya “2016” Imeanza Unasubiri Nini?


“Wakati wa kuvunja mfumo wa tabia zote zinazokuzuia kufanikiwa ni sasa hivi”

 

Mpendwa msomaji wa MAARIFA SHOP; Je! Unaweza kuamini kuwa tayari tumeishafyeka WIKI MOJA ya mwaka mpya wa 2016?
 ... Endapo na wewe huko kama lile kundi la wengi, basi yawezekana tayari umeanza kusahau yale yote uliyokuwa ukipanga kufanya pindi mwaka mpya wa 2016 utakapofika.  
Heee! Kumbe tayari tumo ndani ya meli iitwayo 2016 ambayo.......

Monday, January 4, 2016

Fumbuka Mtanzania

"Imetosha kusherekea 2016 – Twende Kazini!!"

– Leo wakati naamka asubuhi, nilijikuta nikijisemea maneno moyoni bila kutoa sauti yoyote. Maneno ambayo nilijisemea ni “sherehe za mwaka mpya zimeisha na sasa nikwenda kazini tayari kuanza utekelezaji wa malengo yangu ya 2016.

Hapa ninamaanisha – Haijalishi unayo mikakati ya namna gani au umejiwekea malengo makubwa kiasi gani mwaka huu, BADO hutaona mabadiliko ya kweli, iwapo....